MENEJA MKUU - (Marudio)
Job Description
ELCT
ND SACCOS inawatangazia upya watanzania wenye sifa ili kujaza nafasi ya kazi ya
Meneja Mkuu wa Chama. Meneja Mkuu wa Chama atakuwa ndiye Mtendaji Mkuu
na msimamizii wa shughuli zote za Chama na atawajibika moja kwa moja kwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama.
MAJUKUMU YA MENEJA MKUU
Meneja ana jukumu la kusimamia utekelezaji wa shughuli za kila za Chama ambazo ni pamoja na:
MAJUKUMU YA MENEJA MKUU
Meneja ana jukumu la kusimamia utekelezaji wa shughuli za kila za Chama ambazo ni pamoja na:
- Kuhakikisha mifumo ya utendaji kazi na utoaji taarifa ipo madhubuti na inawezesha mawasiliano;
- Kuandaa na kusimamia mpango mkakati, mpango biashara, bajeti ya mwaka na programu ya utekelezaji;
- kuhakikisha malengo na shabaha za Chama zinafikiwa;
- Kushughulikia masuala yote yanayowahusu Watumishi, hususani ajira, utendaji kazi, Nidhamu, mafunzo na uendelezaji wa rasilimali watu;
- Kukiwakilisha Chama katika shughuli na uingiaji wa mikataba;
- Kuhakikisha vitabu vya hesabu vinaandikwa, hesabu zinaandaliwa na kuwasilishwa kwa Wakaguzi kwa wakati;
- Kuhakikisha taarifa ya mapato na matumizi, mizania na taarifa ya mikopo iliyochelewa zimeandaliwa kwa usahihi na kuwasilishwa kwa wakati;
- Kutoa taarifa za Menejimenti kwenye vikao vya Bodi ambazo zinaeleza hali ya kifedha ya Chama ikiainisha mizania, hesabu ya mapato na matumizi, taarifa ya mikopo iliyochelewa, bajeti ya mwaka, mwenendo wa Chama na uwiano wake;
- Kuidhinisha matumizi yaliyopo kwenye makisio kwa viwango vilivyowekwa na Bodi na kutia saini kwenye nyaraka zinazoruhusu utoaji fedha za Chama kwa kuzingatia ukomo ulioainishwa kwenye sera za chama;
- Kuisaidia Bodi kupanga viwango stahiki vya riba, ada na gharama nyingine kwa bidhaa na huduma zitakazotolewa;
- Kuisaidia Bodi katika kubainisha dhamana zinazokubalika na zinazoweza kutumika kudhamini mikopo;
- Kuhakikisha kuwa kuna ukwasi wa kutosha kukidhi mahitaji ya mikopo, uchukuaji wa akiba na gharama za uendeshaji;
- Kusimamia ufunguaji na uendeshwaji wa akaunti za Chama;
- Kusimamia ajira na masuala ya kinidhamu kwa Watumishi walioko katika mamlaka yake;
- Kutoa taarifa stahiki kwa mamlaka zinazohusika kwa muda muafaka;
- Kuitisha Mkutano Mkuu wa Chama baada ya kushauriana na Mwenyekiti;
- Kuwa Katibu katika Mikutano yote Mikuu ya Chama na ya Bodi;
- Kutekeleza mapendekezo yanayotolewa kwenye taarifa za Wakaguzi wa Ndani na wa Nje na taarifa za kiuchunguzi zinazotolewa na Mamlaka husika; Kuhakikisha utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Ushirika, Sheria ya Vyama vya Ushirika Namba 6 ya Mwaka 2013 na Kanuni zake, Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha na. 10 ya mwaka 2018 na Kanuni zake za mwaka 2019 pamoja na Sheria nyingine za Nchi; na
- Kufanya kazi na majukumu mengine kadri ya maelekezo ya Bodi;
Job Requirement
SIFA NA UJUZI
Barua za maombi zielekezwe kwa; MWENYEKITI WA BODI, ELCT ND SACCOS, S.L.P 7779 MOSHI.
Barua za maombi ziandikwe kwa lugha ya Kiswahili na kuwasilishwa kupitia mfumo wa ajira wa Chama (ELCT ND SACCOS AJIRA PORTAL) unaopatikana katika tovuti ya Chama ya www.elctndsaccos.org au www.ajira.elctndsaccos.org Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe16 April, 2025 saa 05:59 Usiku.
![]()
- Awe ni raia wa Tanzania;
- Awe na angalau elimu ya shahada ya kwanza katika Benki, Benki na Fedha, Uhasibu, Uchumi, Menejimenti na Utawala, Fedha na Uwekezaji, Usimamizi wa Vyama vya Ushirika aliyejiimarisha katika Uhasibu, Biashara, Usimamizi wa Biashara aliyejiimarisha katika Uhasibu au fani inayofanana na hizo kutoka katika Chuo kinachotambulika na Serikali;
- Awe na uzoefu katika nafasi ya Uongozi wa Taasisi kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu;
- Awe na ufahamu wa Utawala wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo kwa kuzingatia Sheria zinazosimamia Ushirika na Huduma ndogo za kifedha nchini ; na
- Mwenye Shahada ya uzamili (Masters) katika fani husika atapewa kipaumbele;
- Awe na umri wa kuanzia miaka 30 hadi 50.
- Barua ya maombi ya kazi iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza;
- Wasifu binafsi (CV) ukiainisha anwani na mawasiliano ya uhakika ya wadhamini wasiopungua watatu;
- Nakala za vyeti vya kitaaluma na cheti cha kuzaliwa/uthibitisho wa uraia vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Mahakama;
- Viambatanisho hivi viweke kwenye nyaraka moja ya pdf.
- Mwombaji aoneshe mawasiliano yake bayana;
- Mwombaji atakayeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili;
- Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa kuja kufanya usaili (Nauli, Chakula, malazi nk);
- Mwombaji ambaye hatutawasiliana nae ndani ya mwezi mmoja baada ya tarehe ya ukomo wa kuwasilisha maombi atambue kuwa hakufanikiwa.
Barua za maombi zielekezwe kwa; MWENYEKITI WA BODI, ELCT ND SACCOS, S.L.P 7779 MOSHI.
Barua za maombi ziandikwe kwa lugha ya Kiswahili na kuwasilishwa kupitia mfumo wa ajira wa Chama (ELCT ND SACCOS AJIRA PORTAL) unaopatikana katika tovuti ya Chama ya www.elctndsaccos.org au www.ajira.elctndsaccos.org Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe16 April, 2025 saa 05:59 Usiku.